Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mashujaa FC afuguka kilichowaponza kwa Yanga

Okrah Mashujaa Msj Kocha Mashujaa FC afuguka kilichowaponza kwa Yanga

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mashujaa FC, Abdallah Barres amesema wamefungwa na Yanga SC kisa kutokuwa makini Uwanjani kwani mpaka dakika za mwisho walikuwa wamewamudu vizuri Wananchi.

Bares amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga na kuambulia kipigo cha bao 2-1, mabao ya Yanga yakifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 44 na Mudathir yahya dakika ya 86 wakati bao la Mashujaa likifungwa na Mtumbuka dakika ya 65.

“Wachezaji wangu wamefanya vizuri kama tulivyowaagiza, kilichotokea tumecheza na timu kubwa, wana wachezaji wanaoweza kuamua mchezo. Tumepoteza umakini ndiyo maana wakatuadhibu tukapoteza mchezo.

“Hata hivyo niseme kuwa, kuharibu kwa mechi ya leo kumetokana na uchovu, tumetoka kucheza mechi, tumesafiri kutoka Kigoma kuja huku… Kwa sasa tunajiandaa na mchezo dhidi ya Kigoma tunaamini tutakwenda kupambana na kupata matokeo.

“Kwanza tuliwasoma wapinzani wetu kwenye dakika 15 za kwanza, wana kasi na wanacheza. Kipindi cha kwanza walifanikiwa kupata bao lakini kipindi cha pili tukasema tunaenza kuanza mchezo upya na mbinu mpya, tukawafosi mwisho wa siku tukapata bao.

“Lakini umakini wa wachezaji wangu haukuwa mzuri, yanga wakafunga tena dakika za miwisho tukapoteza mchezo. Sisi tumechukua kama somo kiufundi, kwa vile tumemaizana na hawa wakubwa hivyo tunakwenda kucheza sasa na wale wa level yetu, tunaamini tutafanya vizuri zaidi,” amesema Bares.

Aidha, Bares amewasifia mabeki wake akisema wamecheza vizuri lakini mchezaji wake Bora ni Golikipa wake Erick Johora ambaye amonesha mchezo mzuri akitoa hatari nyingi za Yanga ambazo zingeweza kuzaa mabao mengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: