Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Man United apagawa na kiwango cha Marcus Rashford

FEA9CEC4 8A7F 4D31 8498 F4C1EE021269.jpeg Marcus Rashford na Erik Ten Hag

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford amemkosha kocha wake ndani ya klabu hiyo Erik Ten Hag kutokana na ubora ambao amekua anauonesha kwasasa.

Marcus Rashford ambaye amefunga bao moja leo katika ushindi wa mabao mawili kwa bila walioupata Man United dhidi ya klabu ya Leeds United,Mshambuliaji huyo kwasasa anafanikiwa kufikisha mabao 21 kwenye michuano yote mpaka sasa.

Kocha Erik Ten Hag wakati akizungumza na waandishi wa habari baad ya mchezo dhidi ya Leeds United aliulizwa kama mshambuliaji huyo ni miongoni mwa washambuliaji bora kwasasa barani ulaya na kocha huyo kusema “Ndio ni moja ya washambuliaji wa bora kwasasa barani ulaya na nilivutiwa nae tangu siku ya kwanza. Nilifurahi kufanya kazi na yeye na tunaweza kupata kilicho bora zaidi kwake kwakua ana ubora mkubwa”

Marcus Rashford amekua kwenye ubora mkubwa sana ndani ya msimu huu kwani amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi ndani ya klabu hiyo, Magoli yake yanaonesha ni namna ameimarika na kuweza kuibeba timu hiyo hata timu hiyo inapokua kwenye wakati mgumu.

Mshambuliaji Marcus Rashford ambaye alipewa jukumu la kuhakikisha anafunga magoli 20 msimu huu lakini mpaka sasa ameshafunga mabao 21 kwenye michuano yote huku akiwa na mabao 12 ndani ya ligi kuu ya Uingereza, Hii imeonesha mabadiliko makubwa kwa mchezaji huyo kwani msimu mzima ulimalizika alifanikiwa kufunga mabao matano tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live