Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Man United akuna kichwa idadi ya Majeruhi

Ten Hag Vs Lisandro.jpeg Kocha wa Man United Erik Ten Hag

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Manchester United kinakabiliwa na tatizo la majeruhi kabla ya kumalizika kwa msimu huu baada ya Lisandro Martinez na Raphael Varane kuumia katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sevilla hapo usiku wa kuamkia jana Ijumaa (April 14).

Varane alitoka nje kabla ya mapumziko na Martinez alitolewa nje kwa machela dakika za majeruhi. Sevilla walifunga mabao mawili ya dakika za lala salama na Ten Hag anakabiliwa na matatizo ya uteuzi wa safari ya Nottingham Forest Jhapo kesho huku Marcus Rashford, Luke Shaw, Scott McTominay, Alejandro Garnacho na Donny van de Beek wakiwa tayari nje ya uwanja.

Martinez alionekana kukosa raha wakati akiondoka uwanjani, ingawa Ten Hag alikanusha nyota huyo ali- kuwa ameumia sana.

“Sio eneo hilo, siwezi kujua ni nini lakini sio eneo la kifundo cha mguu,” alisema Ten Hag. “Nadhani hatacheza Jumapili (April 16). Inaonekana hivyo lakini siwezi kusema utambuzi ni nini na napendelea kungoja niseme ni nini.

“Tuna mbadala wazuri sana wa Harry Maguire, Victor Lindelof na Luke Shaw. tuna wachezaji ambao wanaweza kuchukua nafasi zao Martinez na Varane.”

United walifunga mabao mawili katika dakika 20 za mwanzo dhidi ya Sevilla kupitia kwa Marcel Sabitzer huku timu ya Ten Hag ikidhibiti mchezo.

Lakini matokeo duni kipindi cha pili yalimalizika kwa Tyrell Malaciana Maguire kufunga mabao ya kujifunga wenyewe katika dakika sita za mwisho na kuwafanya Wahispania hao wafuzu kwa mkondo wa pili nchini Uhispania juma lijalo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live