Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Man United afunguka mazito

Ole G Solkjaer Ole Gunnar Solskjaer

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United na mchezaji wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer amezungumza kwa mara ya kwanza kwa upana juu ya yaliyokua yanaendelea ndani ya timu hiyo wakati wa uongozi wake.

Ole Gunnar Solskjaer amezungumza mambo mbalimbali ambayo yalikua yanaendelea ndani ya timu hiyo ikiwemo suala la usajili ambao ulikua unafanyika ndani ya timu hiyo kipindi akiwa kocha wa timu hiyo.

Kocha huyo ameorodhesha sajili kadhaa ambazo alizipeleka kwa bodi ya klabu hiyo na kutaka wasajiliwe, Lakini kwa sababu tofauti tofauti bdi ya Manchester United ilishindwa kukamilisha sajili hizo.

Gwiji huyo wa zamani wa Man United amemtaja Earling Haaland kua ni usajili ambao aliupendekeza kabla hata ya mchezaji huyo hajajiunga na Dortmund, Jude Bellingham akiwa Birmingham pia alimpendekeza, Declan Rice alikua akihitajika pia na kocha huyo huku akisema mchezaji huyo hakua anagharimu kiasi ambacho kimewatoka Arsena dirisha lililopita.

Wachezaji wengine ambao Ole Gunnar Solskjaer aliwahitaji ni pamoja na Harry Kane, na Moises Caicedo na kocha huyo ameweka wazi bodi ya klabu hiyo ilimueleza kwa baadhi ya wachezaji hao isingeweza kuwapata kutokana na kutokua na hela ya kutosha kwenye timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live