Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Man United Amsifia Cristiano Ronaldo

Ronaldo Na Kocha Kocha Man United Amsifia Cristiano Ronaldo

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BOSI wa Manchester United, Ralf Rangnick amefunguka juu kiwango ambacho alionyesha staa wake, Cristiano Ronaldo dhidi ya Brighton akisema ni bora kushuhudia tangu atue kikosini hapo.

Rangnick ameanza kuifundisha Man United mwishoni mwa Desemba mwaka jana, baada ya Ole Gunnar Solskjaer kuondolewa.

Man United juzi, ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Brighton mchezo ambao ulipigwa katika Dimba la Old Trafford ukiwa na Premier League.

Katika mchezo huo,Ronaldo alifunga bao na kufuta ukame kwani alikuwa amecheza mechi sita mfululizo bila kufunga.

Rangnick alisema alivutiwa na kiwango cha Ronaldo kwani kilikuwa bora kuliko kawaida tangu atue kikosini hapo na kuanza kuinoa timu hiyo.

“Kiwango cha Cristiano kilikuwa bora sijapataona tangu nimekuwa naye hapa na alikuwa bize akishirikiana na wenzake kuona kila kitu kinaenda sawa.

“Nafikiri hata wiki iliyopita alikuwa bora ila sio kwa kiwango hiki na ndiyo maana ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chetu.

“Kitu muhimu sio kufunga tu bali amefunga bao zuri na bora ambalo lilikuwa muhimu kwetu kama timu jambo ambalo ni muhimu na tumefanikiwa kuondoka na clean sheet,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live