Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mamelodi awajibu wanaombeza

Aziz Mokwena 2681708 Kocha Mamelodi awajibu wanaombeza

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Sekhukhune kumalizika kwa mabao 2-1, Kocha wa Mamelodi Mokwena alipata nafasi kuuzungumzia mchezo wao wa kesho wa nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance De Tunis, katika dimba la Loftus Versfeld akisema.

Baada ya kufungwa na ES Tunis kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza, Mamelodi Sundowns watashuka Dimbani kesho kukipiga na miamba hao wa soka wa Tunisia kesho 26 Aprili majira ya saa 2:00 nchini Afrika Kusini.

“Ligi ya mabingwa ni ligi ya mabingwa, nilikuwa kocha msaidizi wa kocha aliyepita kwa muda mrefu, kocha aliyepita alitimia miaka 8 kupambana kupata taji la Champions League na alibeba mara moja tu, alicheza Nusu fainali mara mbili na moja tu tulifika fainali.

“Kwangu huu ni msimu wa pili kama kocha na tumecheza nusu fainali mbili, kuna wakati napata hisia kwa kuona watu hawathamini hiko,” amesema Mokwena.

Mwisho ametolea mfano Manchester City licha ya uwekezaji mkubwa juzi wametolewa na Real Madrid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live