Kocha Mkuu wa Mamelodi, Rulani Mokwena amefunguka kuhusu mipango yake kuelekea mechi ya Robo Fainali ya CAFCl dhidi Yanga SC itakayopigwa Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa na malengo yake ya kuchukua kila taji lililopo mbele yake msimu huu.
Mokwena amefunguka hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa NedBank Cup nchini Afrika Kusini ambapo Mamelodi Sundowns walishinda 2-0 dhidi ya Martzburg United.
Ikimbukwe kibarua kikubwa kinachofuata ni mechi yao dhidi ya Yanga katika michuano ya CAF Champions League.
"Hapana siwezi, nipo kwenye nafasi ngumu kuzungumzia kuhusu kubeba kila taji lililo mbele yangu, nachofikiria ni mechi inayokuwa mbele yangu, ninapambana kushinda kila mchezo unaokuwa mbele yangu.
"Kwa sasa nimeelekeza akili yangu kwenye mchezo ujao (dhidi ya Yanga) na leo ni siku ya upembuzi (analysis) kwa ajili ya kupitia na kuangalia mapungufu yetu ili kuyarekebisha. Kuna makossa mengi ambayo tuliyafanya hata tulivyokuwa tukicheza na Chippa, kwa hiyo nina wakati wa kufanya masahihisho kwenye baadhi ya makossa ambayo tumeyafanya katika mechi za Ligi yetu ya Super Sport.
"Kwa hiyo tuna mambo mengi ya kufanya kwenye haya mapumziko ya FIFA. Inahitaji muda lakini tunaamini kila kitu kitakwenda sawa na wachezaji watarejea kwenye utimamu wao polepole kabla ya mechi ya Yanga," amesema Mokwena.