Kocha wa Mlabu ya Mamelodi, Rhulan Mokwena amesema kuwa hawakufanya maandalizi ya kutoka kuelekea mchezo wao wa robo fainali ya CAFCL Machi 30, 2024 dhidi ya Yanga ndio maana walishindwa kupata ushindi.
Mokwena amesema kuwa asilimia kubwa ya wachezaji wake tegemezi walikuwa timu ya taifa hivyo hawakufanya mazoezi ya kutosha na klabu huku akibainisha kuwa kumkosa nahodha wake, Thba Zwane ni sababu nyingine ya mchezo huo kuwa mgumu kwao.
"Kama nilivyoongea kwenye press baada ya mechi. Tulitarajia tutashinda dhidi ya Yanga, hatujashinda kwa sababu Yanga walicheza vizuri lakini pia wachezaji wetu wengi walikuwa kwenye timu ya Taifa hivyo hatukupata muda wa kutosha kujiandaa, hatukuwa na chemistry nzuri.
"Pia tulimkosaThemba Zwane ni Nahodha wa Timu, Ni mchezaji muhimu kwenye kikosi ingawa siwezi kusema kukosekana kwake ndio chanzo cha kutopata matokeo mazuri kwenye mchezo wa awali.
"Wachezaji wote walipambana hasa kipindi cha pili, acha tuone kitakachotokea mchezo ujao Pretoria naamini tutashinda japo mechi haitakuwa rahisi," amesema Mokwena.
Mamelodi na Yanga watarudiana Ijumaa ijayo Aprili 5, 2024 katika Dimba la Loftus Versfeld mjini Pretoria nchini Afrika Kusini baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa kumalizika kwa sare ya bila kufungana.