Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha: Makipa Dodoma Jiji wepesi

Kipa Dom Kocha: Makipa Dodoma Jiji wepesi

Fri, 5 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa zamani wa makipa wa Dodoma Jiji Mfaume Athumani ameishauri kama itabaki Ligi Kuu Bara msimu ujao inapaswa kuangalia vizuri eneo la golini kwani msimu huu limekuwa na changamoto ya makipa kuruhusu mabao mepesi.

Kwa sasa Klabu hiyo ina makipa watatu ambao ni Daniel Mgore, Rahim Sheikhe na Aron Kalambo.

Mfaume ambaye amewahi kucheza Soka kulipwa Uarabuni pia amezichezea timu za Majimaji, Waziri Mkuu, Kurugenzi na CDA za Dodoma.

Dodoma Jiji katika michezo 27 iliyocheza mpaka sasa imeruhusu mabao 33 huku ikifunga 22. Mfaume awewahi kuifundisha timu hiyo akiwa na Mbwana Makata na Renatus Shija pia amewewahi kuzifundisha timu za Ashanti,Coastal Union,Tanzania Stars,Singida United na Timu ya Taifa ya Vijana Under 23 kama kocha wa makipa.

Mfaume alisema ameifuatilita Dodoma Jiji na kugundua inachangamoto ya kuruhusu mabao mepesi hivyo kama itabaki kwenye ligi ilifanyie kazi jambo hilo na katika michezo iliyobaki.

“Aron ni kipa mzuri sana lakini nahisi kama anakuwa hana ufiti Dodoma Jiji inafungwa mabao marahisi sana hili waliangalie kama watabaki kufanya aina ya usajili ambao utaondoa tatizo hilo,”alisema kipa huyo wa zamani.

Kuhusu viwango vya makipa katika ligi Kuu Mfaume alisema : “Bado bado kuna makosa mengi bado hawatimizi wajibu wao kila ukiangalia ligi lazima ukute kuna makosa ya makipa, bado tuna safari ndefu ya kupata makipa ambao hawatafanya makosa katika michezo mitatu mfululizo”.

Timu hiyo inaendelea na tizi kujiandaa na michezo mitatu iliyosalia ya Ligi Kuu Bara ambayo yote itacheza ugenini ukiwemo dhidi ya Yanga.

Timu hiyo inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 katika michezo 27 iliyocheza mpaka sasa.

Katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo,timu hiyo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC lilofungwa na Collins Opare.

Timu hiyo imebaisha michezo dhidi ya Yanga (Benjamini Mkapa),Namungo (Kassim Majaliwa) na Ruvu Shooting ( Mabatini).

Mwanaspoti lilishuhudia wachezaji wa timu hiyo wakifanya mazoezi juzi katika uwanja wa Kilimani yaliyoongozwa na Kocha Melis Medo na msaidizi wake Kassim Liyogope.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo,Liyogope alisema licha ya kufanya maandalizi hayo bado hawajajua watacheza lini ya Yanga. “Tunajiandaa lakini bado hatujapata ratiba tunacheza lini na Yanga maana ndio mechi yetu inayofuata.

“Sisi ni askari muda wote tunatakiwa kuwa tayari, tupo tayari ndio maana unaona tunaendelea na mazoezi, dhamira yetu ni kufanya vizuri katika michezo iliyobaki,”alisema kocha huyo.

Beki wa kushoto wa timu hiyo,Abubakari Ngalema alisema licha ya kushinda mchezo uliopita lakini bado hawapo katika nafasi nzuri hivyo watapambana kuhakikisha wanapata matokeo katika michezo iliyobaki.

Ngalema ambaye pia humudu kucheza nafasi ya winga alisema wanajua mashabiki wa timu hiyo wanachotaka ni timu hiyo isishuke daraja hivyo watapambana kuhakisha wanainusuru na janga hilo.

Chanzo: Mwanaspoti