Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Liverpool agoma kung'oka

Jurgen Klopp Winner Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa kikosi cha Liverpool Jurgen Klopp (55) amesema bado yupo sana na hana mpango wa kuondoka klabuni hapo japokuwa wanapitia katika kipindi kigumu kutokana matokeo wanayoyapata msimu huu wa Ligi Kuu ya England.

Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani amesema hana mpango kuondoka kwa sasa ndani ya kikosi hicho japokuwa wamekuwa wakipitia changamoto ya kukosa matokeo mazuri.

“Kama ungekuwa msimu wangu wa kwanza kuinoa Liverpool, ningeweza kufanya maamuzi mengine.”

“Ninatarajia kuendelea kuwepo kutokana hapa kutokana na mazuri niliyoyafanya hapo awali, sitaondoka kwa sababu ya kufanya vibaya msimu huu,” amesema.

“Tuna wamiliki ambao wanatambua ugumu wa matokeo ambayo tunayapitia kwa sasa, haina haja ya kuanza kujilaumu, nina imani tutafanya vizuri zaidi msimu ujao.”

“Ninatambua nitaendelea kuwepo katika kikosi cha Liverpool kutokana na kilichotokea hapo awali,” amesema.

Klopp tayari aliishaipatia Liverpool mafanikio makubwa ikiwemo kubeba mataji katika kipindi cha miaka saba na nusu aliyokaa Anfield.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live