Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Kagera Sugar atamba kuifunga Simba SC

Image 160 1140x640.png Kocha Kagera Sugar atamba kuifunga Simba SC

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime ametamba kuifunga Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam keshokutwa Ijumaa (Desemba 15).

Akizungumza jijini humo Kocha Maxime amesema kinachompa matumaini ya kushinda mchezo huo ni wakati mgumu wanaopitia Simba SC kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Simba SC ni timu yenye wachezaji wazuri, hilo hatulipingi lakini kuhusu uzoefu hata Kagera Sugar tuna uzoefu wa kutosha cha msingi tumejipanga kupata pointi tatu katika mchezo huo bila kujali tunacheza wapi na timu gani,” amesema Maxime.

Amesema ameifuatilia Simba SC katika mechi nyingi za Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na anajua mapungufu waliyonayo ambayo amewaelekeza wachezaji wake mazoezini.

Amesema hawapo tayari kupoteza mechi mbili mfululizo baada ya wiki iliyopita kufungwa na Coastal Union wakiwa ugenini Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Kagera Sugar inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 13 katika michezo 11 walizocheza na Simba SC inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 19 katika michezo nane waliyocheza, wakishinda sita, sare moja na kupoteza moja.

Chanzo: Dar24