Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha KMC: Tunakwenda kucheza na Yanga ngumu

Abdoul Moalin Sfd.jpeg Abdoul Moalin

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa KMC, Abdoul Moalin amesema mechi dhidi ya Yanga ni ngumu na wanakwenda kucheza na timu inayotetea taji.

Abdoul Moalin amesema hayo leo wakati akizungumza na wahabari kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga utakaopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

"Tunaenda kucheza na Yanga ambayo ni timu ngumu kupata matokeo, ni Mabingwa wa Ligi msimu uliopita na wanafanya vyema kimataifa.

"Kwetu KMC tunatakiwa kuwa bora dhidi yao ili kupata matokeo, kikubwa ni kufocus zaidi na mchezo ili tuweze kupata matokeo Mazuri," amesema Abdoul Moalin.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: