Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Jwaneng Galaxy achukia kuambiwa waipiga Wydad kishirikina

Morena Ramoreboli.jpeg Morena Ramoreboli.

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Jwaneng Galaxy, Morena Ramoreboli juzi aliamua kuondoka kwenye mkutano na Waandishi wa habari baada ya mwandishi mmoja kumuuliza kuwa wameshinda mchezo wao dhidi ya Wydad Casablanca kwa ushirikina.

Mwandishi: "Inaonekana Jwaneng Galaxy imeifunga Wydad kwa kutumia uchawi."

Morena Ramoreboli alijibu: “jamani, hamjatutendea haki sisi. Ah, sasa mnatushushia heshima, mnasema tumeshinda kwa sababu ya mambo ya ushirikina! Msitudharau!” amesema Morena Ramoreboli.

Baada ya kutoa kauli hiyo, Morena Ramoreboli alichukulia kauli hiyo kama dharau dhidi ya timu yake.

Jwaneng Galaxy juzi ilishinda mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwafunga Wydad kwa bao 1-0 nchini Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live