Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Julio azungumzia makundi U-20

D9f3b0e6566fdbd16db462a83c5beede Kocha Julio azungumzia makundi U-20

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa timu ya taifa ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelu au Julio amesema maandalizi ya uhakika ndio njia pekee ya vijana wake kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika.

Julio aliyasema hayo jana baada ya Shirikisho ka Soka Afrika (Caf) kutangaza makundi ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri huo yatakayofanyika Mauritania, ambapo Tanzania iko Kundi C pamoja na Ghana, Gambia na Morocco.

Fainali hizo zitafanyika kuanzia Februari 14 hadi Machi 4, ambapo wenyeji Mauritania watafungua dimba dhidi ya Cameroon katika mchezo utakaofanyika katika jiji la Nouakchott.

Alisema makundi yote yako sawa na kikubwa ni maandalizi ya mapema na tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeiweka timu hiyo kambini, hivyo alitaka serikali kupitia Wizara ya Michezo kusaidia ili wapate mechi nyingi za majaribio za kimataifa.

Kwa mujibu wa Msemaji wa TFF, Clifford Ndimbo, timu hiyo imepiga kambi Arusha ikijiandaa kwa mashindano hayo ili kuhakikisha inafanya vizuri.

Julio alisema hata hao wanaoitwa vigogo wa soka kama Ghana, Gambia na Morocco nao walianzia chini, lakini sasa wako vizuri, hivyo na Ngorongoro Heroes itafika huko waliko wengine kama itaandaliwa vizuri.

Alisema anapendelea timu yake ipate mechi nyingi za kimataifa za majaribio ili iweze kujiandaa na kwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo ya Afrika bila kujali inakutana na timu gani.

Ratiba hiyo ya makundi ilipangwa jana katika jiji la Yaounde, Cameroon ambako fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan 2020, zinaendelea. Kundi A: Mauritania, Cameroon, Uganda na Msumbiji Kundi B: Burkina Faso, Tunisia, Namibia, Afrika ya Kati Kundi C: Ghana, Tanzania, Gambia na Morocco.

Chanzo: habarileo.co.tz