Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha JKU afunguka ishu ya Feisal Salum

Kocha JKU Afunguka Ishu Ya Feisal Salum Kocha JKU afunguka ishu ya Feisal Salum

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: dar24

Baada ya Kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kuonekana akiitumikia JKU katika mchezo wa Kirafiki dhidi ya Mlandege jana Alhamis (Desemba 29), Kocha wa Maafande hao wa Jeshi la Kujenga Uchumi Sheha Khamis amefunguka kuhusu mchezaji huyo.

Feisal amekua gumzo kwa sasa kufutia sakata lake la kuandika Barua ya kuondoka Young Africans huku Klabu ya Azam FC ikitajwa kuwa mbioni kumsajili.

Kocha Sheha ambaye jana alimtumia Feisal katika mchezo ambao ulimalizika kwa JKU kuibuka na ushindi wa mabao 4-2, amesema:

“Kwanza (Feitoto) yupo sawa, hana presha yoyote kama ilivyo mtandaoni ambapo mashabiki wanasema mengi, halafu anaipenda Yanga, kinachomsumbua ni wakati huu ambapo ana nguvu na yupo kwenye kiwango haoni maslahi yanayomstahili.”

“Sababu kubwa ya kutaka kuondoka anataka jasho lake liende kihalali, pia anajua wanaomshangilia leo, kesho atakapokuwa na maisha magumu watamzomea, hilo ndilo analoliwaza zaidi tofauti na wanavyomchukulia baadhi ya watu ambao hawajajua ukweli wa mambo na hawajakaa naye akawaeleza.”

“Ninachowashauri Yanga kama wazazi wangekaa naye chini na siyo kutumia nguvu nyingi kwenye mitandao ya kijamii, pia wakumbuke Fei huyohuyo ndiye alikuwa nao nyakati za dhiki kwa nini wanapopata hawaoni hilo.”

Chanzo: dar24