Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha JKT aanika madhaifu ya Azam, aliwabana hapa

Azam Hamad Ally Kocha JKT aanika madhaifu ya Azam, aliwabana hapa

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Hamady Ally amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kupata sare dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa jana katika Dimba la Meja Jenerali Ismhuyo, Mbweni Dar es Salaam.

Hamad ameanika mbinu aliyoingia nayo na kufanikiwa kuwadhibiti Azam FC ambao walimaliza msimu uliopita katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

“Tumecheza mchezo mgumu na timu ngumu ambayo imetoka kucheza CAF Champions League, Azam kwa sasa ni timu bora kila idara na wana mwalimu ambaye alikuwepo msimu uliopita na mpaka sasa ameendeleza kile alichokianza msimu jana.

“Mimi ni kocha mpya JKT, falsafa mpya na tunaangalia jinsi gani ambavyo tutaweza kufanya kazi. Kwa wiki sita ambazo nimezipata nina furaha kwa kile ambacho vijana wamekionesha leo na ninaona kuna maendeleo mazuri yanakuja kadri tunavyojiandaa kwa michezo mingine.

“Tulitarajia kupata alama tatu lakini tumepata alama moja sio mbaya lakini wachezaji wamejitoa na wameonesha kitu kikubwa sana, ninaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi ya hapo.

“Kila mchezo una mbinu yake na kuona aina ya mshambuliaji ambaye unaweza kumuweka, ukiangalia Azam mabeki wao hasa mabeki wa kati wawili, wana madhaifu kwenye kukimbia kwa hiyo niliweka wachezaji wazuri kwenye kukimbia ili kuzitumia nafasi za transition (kutoka kukaba kwenda kushambulia). Hiki ndicho kilisababisha nisiwatumie Bocco ama Lyanga, kuna mechi itamhitaji Bocco na mechi nyingine itamhitaji Lyanga,” amesema Hamady Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live