Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha JKT: Kila mtu ashinde mechi zake

JKT Queens Kikosi cha JKT Queens

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

JKT Queens inazidi kuwatimulia vumbi mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) Simba Queens huku kocha wa maafande hao Ali Ali akisema kuwa hakuna namna kila mtu ashinde mechi zake.

Maafande hao wameonekana wamepania msimu huu kutwaa ubingwa kwani wanakwenda jino kwa jino na Simba na juzi waliichapa The Tigers mabaoa 6-0 na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na pointyi 37.

Hata kama Simba walishinda mechi yao ya jana jioni dhidi ya Amani Queens watafikisha pointi 36 na kuwa nyuma ya JKT Queens kwa pointi moja.

Licha ya kwamba JKT Queens ana mechi mbili ngumu kati ya tatu alizobakiwa nazo dhidi ya Yanga Princess (Mei 3) na Fountai Gate(Mei 10) na Mkwawa (Mei 17) kabla ya msimu kumalizika lakini kocha Ali anaamini kama wakipambana kila kitu kinawezekana.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya JKT na Fountain timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 huku maafande hao pia wakitoka suluhu na Yanga Princess katika mchezo wa kwanza.

"Hivi sasa kilichobaki ni kila mtu kushinda mechi zake tu hakuna cha kusema namuombea mabaya fulani apoteze ndio mimi nipate ubingwa hilo kwetu halipo, hapa ni mwendo wa kupambana na kushinda.

"Najua tumebakiwa na mechi ngumu lakini sisi ni wanajeshi lazima tupambane kwa uwezo wetu kuhakikisha tunashinda mechi zote zizliobaki na kutwaa ubingwa msimu huu ili kurudisha heshima ya timu yetu, "alisema Ali.

Mara ya mwisho JKT Queens kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ilikuwa msimu wa 2017/2018 na 2018 / 2019. Mabingwa watetezi Simba baada ya mchezo wa jana jioni watakuwa wamebakiwa na michezo mitatu dhidi ya Alliance Girls , Baobab Queens na Ceasiaa Queens ili kujua kama watatwaa tena ubingwa au watauachia.

Chanzo: Mwanaspoti