Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Ihefu akubali mziki wa Simba, Baleke

Zubery Katwila Kocha wa Ihefu zuberi Katwila

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ihefu juzi ilikubali yaishe kuendelea kuwa wanyonge mbele ya Simba kwa kukubali kulazwa mabao 2-0 ikiwa ni kipigo cha sita mfululizo tangu waanze kukutana kwenye mashindano yote.

Timu hiyo ambayo ilikuwa gumzo kwa mechi za karibuni ikishinda michezo yake, haikuamini kilichowakuta kwenye uwanja wao Highland Estate Mbarali walipojikuta wakifungwa mabao 2-0 dakika za lala salama.

Mshambuliaji Jean Baleke ndiye alipeleka kilio tena kwa vijana hao wa Mbarali ikiwa ni siku chache alipowakanda mabao matatu wakati Simba ikitakata 5-1, katika mechi ya Kombe la Shirikisho (ASFC), Uwanja wa Chamazi.

Kabla ya mchezo huo wa juzi Jumatatu, Ihefu ilikuwa imecheza mechi nne za ligi kuu bila kupoteza ikishinda tatu na sare moja na kuwa nafasi ya sita kwa pointi 30.

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Zubery Katwila alikubali matokeo hayo akisema vijana wake walikosa umakini katika kutumia nafasi walizopata na kwamba bado hawajakata tamaa.

Alisema benchi la ufundi linaenda kukaa upya na kurekebisha makosa haswa eneo la ushambuliaji na beki kuhakikisha mechi zilizobaki wanashinda na kumaliza nafasi nzuri kwenye msimamo.

“Mechi ilikuwa ngumu kwa sababu kila timu ilihitaji ushindi, wapinzani walifanikiwa kutumia nafasi walizopata tofauti na sisi tulioshindwa, tunakubali lakini tunaenda kujipanga upya na mechi zijazo tufanye vizuri,” alisema Katwila.

Aliwaomba mashabiki na wadau wa soka wilayani Mbarali kutokata tamaa na kwamba Ihefu itaendelea kuwapa raha akisema michezo iliyobaki wanaamini watashinda yote.

Chanzo: Mwanaspoti