Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Ihefu afunguka kilichowaponza kwa Yanga

Yanga Aziz WA0007 Kocha Ihefu afunguka kilichowaponza kwa Yanga

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Kikosi cha Ihefu Mecky Mexime amezungumza na Wana habari baada ya kupoteza Mchezo dhidi ya Yanga na kueleza ugumu wa Mchezo huo na sababu za yeye kupoteza.

Ihefu imepoteza mchezo huo dakika ya 110 kwa bao la Aziz Ki baada ya dakika 90 kutamatika bila kufungana zinaongezwa dakika 30.

“Tunasikitika kwa sababu tumetoka lakini tumepambana vizuri. Mechi ilikuwa kiufundi zaidi lakini ni makosa machache tu yametugharimu tukafungwa bao moja.

“Uwanja sote tumecheza humo humo, labda tungeleta magodoro tuyatandike ndipo ungekuwa tofauti lakini uwanja ndio huo huo. Mimi kwa sababu nimefungwa siwezi kusigizia uwanja, wachezaji wangu wamecheza vizuri, siwadai.

“Mchezo ulikuwa mzuri sana, ukiwalaumu wachezaji utakuwa huwatendei haki, tumepeta chance sisi tena nzuri kuliko wao, lakini hatukuzitumia wao wamezitumia wakatufunga. Wachezaji wamenipa kile ambacho nilikuwa nakitaka. Nadhani hata watazamaji wamefurahi," amesema Mexime.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live