Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha: Harambee Stars imejipata

Timu Ya Harambee Stars Ya Kenya Yaicharaza Sychelles 5 0 Kocha: Harambee Stars imejipata

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Harambee Stars Benson Omala amesema kuwa analenga kuyafunga mabao mengi zaidi baada ya kung’aa kwenye ushindi dhidi ya Ushelesheli Jumatatu usiku.

Harambee Stars ilichapa Ushelisheli 5-0 katika katika uga wa Stade Felix Houphoiet-Boigny jijini Abidjan Cote d’Ivoire na kujipatia alama tatu kwenye Kundi F.

Hii ilikuwa baada ya kutandikwa 2-1 na Gabon mnamo Alhamisi wiki jana. Katika mechi dhidi ya Ushelesheli nahodha Michael Olunga alifunga mabao mawili huku Masud Juma, Omala na beki wa Gor Mahia Rooney Onyango ambaye alichezeshwa kama kiungo, wakifunga bao kila moja.

Harambee Stars ilitarajiwa kutua nchini jana usiku kutoka Abidjan huku mashabiki nao wakiendelea kumiminia timu hiyo sifa kedekede kwa ushindi huo mkubwa.

Omala ambaye amekuwa akipuuzwa na kocha Enjin Firat aliingia mahali pa Masud Juma zikiwa zimesalia dakika 20 na kufunga bao baada ya kumegewa pasi safi na Rooney Onyango.

Mshambuliaji huyo ndiye anaongoza orodha ya ufungaji bao kwenye Ligi Kuu (KPL) akiwa akiewa amecheka na nyavu mara saba.

“Ninafurahi kuwa hatimaye nimefunga goli langu la kwanza kwa timu ya taifa. Nashukuru kocha kwa kunipa nafasi na sasa nalenga kuhakikisha kuwa nafunga katika mechi zijazo za kimataifa, nafunga magoli zaidi,” akasema Omala, wakati wa mahojiano na Taifa Leo.

Omala, 22, anaonekana kuwa mwanasoka ambaye atavumisha Stars siku zijazo hasa katika mashindano hayo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 pamoja Kombe la Afrika mnamo 2027.

Aidha, Firat alimiminia Omala sifa, akisema kuwa alicheza vizuri na anahitaji kujiimarisha zaidi ili kuwa wembe kufungia Kenya magoli mengi katika mashindano yajayo.

Kando na Omala, Mturuki huyo pia alimiminia sifa beki Dennis Ngang’a ambaye alichezea Harambee Star kwa mara ya kwanza akisema aliwazima washambuliaji wa Ushelisheli na pia dhidi ya Gabon ambapo walishindwa 2-1.

Wakati huo huo, Firat amesema ushindi huo dhidi ya Ushelesheli umeweka Stars pazuri kupigania nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Dunia mara ya kwanza katika historia yake.

Timu itakayomaliza nambari ya kwanza kwenye Kundi F itafuzu moja kwa moja kwa Kombe la Dunia.

“Nina hakika hii timu hii itaenda mbali kwa kwa sababu kila mchezaji anaelewa kile kinachoendelea. Nafikiria kuwa soka ya Kenya sasa inaelekea pazuri,” akasema Firat.

“Watu wasisahau kuwa tumecheza mechi mbili ugenini katika kundi letu. Hata dhidi ya Gabon tulicheza vizuri ila hatukuwa na bahati.

Kwa sasa kila mtu anaelewa kuwa Kenya imepiga hatua kisoka na si nchi ambayo ilikuwa chini zamani,” akaongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live