Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Gwambina ajivunia mafanikio kwa muda mfupi

Gwambiiii Pic Data Kocha Gwambina ajivunia mafanikio kwa muda mfupi

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA mpya wa Gwambina, Mohamed Badru amesema kwa muda mchache aliokuwa amekaa katika kikosi cha timu hiyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Badru alisema kabla ya kuanza kazi katika kikosi hicho kilikuwa kimetoka kufungwa mechi tano mfululizo

walishindwa hata kupata sare.

Alisema Gwambina hawakuwa na matokeo mazuri katika mechi zao za nyumbani wala ugenini pengine ndio maana

waliamua kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi na kunichukua.

"Baada ya kuichukua timu kazi ya kwanza ambayo nilifanya ni kutengeneza akili za wachezaji ambazo zilikuwa chini

Related Fundi anatua Yanga Amunike amkumbuka Magufuli Luis: Kaeni chonjona hata morali hawakuwa nayo kutokana na matokeo mabaya mfululizo," alisema.

"Nilifanikiwa katika hilo na ndani ya siku mbili kabla ya kucheza na Kagera Sugar niliwaelekeza kwanza darasani

na siku moja kabla ya mchezo tulikwenda kufanya mazoezi ya uwanjani.

"Nikiwa katika timu ndani ya siku ya tatu mchezo wangu wa kwanza na Kagera tukiwa ugenini nikafanikiwa kupata

sare baada ya kupoteza mfululizo," alisema Badru.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz