Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Gwambina: Kama sio Simba basi Yanga

Gwambina Pic Data Mbonde: Simba hii haishikiki

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TIMU tatu za Yanga, Simba na Azam ndio zipo katika mbio za ubingwa msimu huu kutokana na pointi zao ambazo wamezikusanya katika mechi mbalimbali tangu msimu kuanza.

Yanga ndio vinara wa ligi katika msimamo wamecheza mechi 23, wameshinda 14, wametoka sare nane, wamefungwa moja, wamefunga mabao 36, wamefungwa mabao 14 wamekusanya pointi 50.

Simba wapo katika nafasi ya pili wakiwa wamecheza mechi, 20 wameshinda 14, wametoka sare nne, wamefungwa mbili, wamefunga mabao 45, wamefungwa sita na pointi ambazo wanazo ni 46.

Matajiri wa ligi, Azam FC wamecheza mechi 24, wameshinda 12, wametoka sare nane, wamefungwa nne, wamefunga mabao 34, wamefungwa mabao 17, wamekusanya pointi 44.

Kutokana na msimamo huo wa ligi ulivyo, kocha wa Gwambina, Mohammed Badru amesema kutokana na kikosi cha Simba kilivyo ndani na nje ya uwanja kinaweza kubeba ubingwa mwingine msimu huu.

Badru wakati akihojiwa na Mwanaspoti katika ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd zilizopo Tabata jijini hapa amesema ukiwaangalia wachezaji wa Simba wanaubora na viwango vya juu wale ambao wanaanza katika kikosi cha kwanza na ambao watakuwa benchi.

"Simba wanacheza katika maelekezo ya kocha vile ambavyo anataka kulingana na wapinzani walivyo na likishindikana hilo utaona uwezo wa wachezaji binafsi unaamua mechi," alisema.

"Ukiwaondoa hao labda Yanga naweza kuwapa nafasi za mbio za ubingwa msimu huu lakini timu nyingine zote zinalingana katika aina ya uchezaji wao pamoja na ushindani ambao wanautoa," anasema Badru.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz