Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Gor Mahia achimba mkwara mzito

Jonathan McKinstry Kocha wa Gor Mahia Jonathan McKinstry

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Gor Mahia Jonathan McKinstry amewataka wachezaji wake kuongeza ubora na kujituma ili waweze kushindania taji la Ligi Kuu nchini Kenya KPL.

Kocha McKinstry amesema hayo baada ya timu yake kudondosha alama mbili kufuatia sare ya bao 1-1 na Kariobangi Sharks, ikiwa ni mara ya kwanza wanashindwa kuondoka na alama tatu msimu huu baada ya kushinda mechi mbili za awali za Nzoia Sugar na Bidco.

Wakiwa vinara wa kubeba taji la Ligi mara nyingi zaidi, Gor Mahia walitangulia kupata bao kipindi cha pili kupitia kwa Benson Omala kabla ya kuruhusu Tyson Otieno kusawazisha bao hilo akitumia makosa ya walinzi wa K’Ogalo.

“Dakika chache baada ya kufunga goli tulipoteza hali ya kujiamini, hatukucheza kama sisi tena, kila mmoja alikuwa vibaya. Lazima tubadilike”, alisema kocha McKinstry ambaye ni raia wa Ireland.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live