Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Geita ajiandaa kutimka

Geita Gold Queens Kocha Geita ajiandaa kutimka

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Matokeo mabaya waliopata Geita Gold Queens kwenye mzunguko wa kwanza yameshtua kocha wa timu hiyo, Sultan Juma anayetaka kuacha mikoba.

Geita na Bunda ndio timu zilizopanda msimu huu na hazijaanza vyema kwenye ligi hususani Geita iliyokusanya pointi nne kwenye mechi tisa.

Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo yuko mbioni kuachana nayo ili kutafuta maisha mengine.

Aliongeza sababu ya timu hiyo kutofanya vyema ni maandalizi hafifu ya kuanza msimu yakichagizwa na usajili mbaya ambao umefanywa.

“Mwanzo wakati timu inaanza kufanya vibaya niliwaeleza sababu wakasema dirisha dogo watasajili wachezaji, timu ikakumbwa na majanga ya kifedha ikashindikana, hivyo kwa sasa nipo masomoni lakini nikirudi nafikiri nitamalizana nao,” alisema na kuongeza

“Sababu nyingine wafanyakazi hatujalipwa mishahara tangu mwezi wa 12 hadi leo hilo nalo linaweza kuwa sababu ya timu kutofanya vizuri.”

Chanzo: Mwanaspoti