Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Geita Gold atuliza upepo

Geita Gold Tambo Kikosi cha Geita Gold

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Mathias Wandiba amesema nyota wake hawawezi kuathirika kisaikolojia na kichapo cha kushtua dhidi ya Tanzania Prisons kwani wamekomaa na wameiva kwa ajili ya mashindano makubwa kama Ligi Kuu.

Geita Gold ambayo ilikuwa haijafungwa katika Uwanja wa Nyankumbu kwa zaidi ya mechi 35 tangu msimu wa 2020-2021, Jumatatu ilishangazwa baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Tanzania Prisons. Timu hiyo yenye maskani yake mkoani Geita inakamata nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 baada ya michezo 27 ikishinda tisa, sare 10 na kupoteza nane, mchezo ujao itavaana na Mbeya City katika uwanja huo.

Wandiba aliliambia Mwanaspoti kuwa kikosi chake kina wachezaji mahiri, wenye uzoefu na Ligi Kuu ambao wameandaliwa kushindana katika mazingira yoyote ambapo licha ya kupoteza mchezo wanakaa chini kujitathmini na kusonga mbele.

Kocha huyo wa zamani wa Mbeya City na mchezaji wa Pamba, alisema wanarudi kwenye uwanja wa mazoezi kutazama makosa yalikuwa wapi ili wafanye marekebisho na kurudi imara zaidi kwenye mchezo ujao dhidi ya Mbeya City.

“Mchezo na Tanzania Prisons, safu yetu ya ulinzi ilifanya makosa wenzetu wakayatumia na kufunga lakini ndiyo mchezo wa soka cha msingi tunajiandaa na mchezo ambao uko mbele yetu ili tupate matokeo mazuri,”

“Naamini wachezaji hawatoathirika kisaikolojiaa mchezaji hadi unafika ligi kuu naamini umeshakomaa, tutarudi mazoezini tutaangalia makosa yalikuwa wapi tutaweka akili yetu sawa na kujiandaa na mchezo unaokuja,” alisema Wandiba

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: