Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Gamondi alivyomgomea Eng. Hersi

Hersi Gamondi Mz Kocha Gamondi alivyomgomea Eng. Hersi

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa uamuzi wa kuipeleka timu yake nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi (pre-season) yalikuwa magumu kwani hata kocha Mkuu, Miguel Gamondi alikuwa amekataa mwanzoni kabla ya kukubali baadae.

Hersi amesema hayo baada ya Yanga kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Toyota Cup kwa kuwabamiza wenyeji Kaizer Chiefs kwa bao 4-0 nchini mwao jana Jumapili, Julai 28, 2024.

"Kuja Afrika Kusini kulikuwa na ugumu wake na wepesi wake. Kiufundi timu ilitakiwa kubaki Dar na kujiandaa kama ambavyo tulikuwa tumepanga na ilikuwa ngumu kwa mwalimu kukubali kuleta timu hapa kwa sababu alitamani aendelee kubaki pale kuisuka timu.

"Sisi kama viongozi tulikuwa tunapigania upande wa kuipa exposure klabu yetu. Leo sote tunaona tumepata nafasi ya technical training kwa maana ya pre-season na kuchezesha timu yetu, kuiuza nje ya Tanzania. Tumecheza na timu kutoka Ujerumani, ni kiwango wa juu sana cha ubora. Leo Yanga imefahamika Afrika na Ujerumani kwa hiyo tumeiuza klabu yetu kwa kuitangaza.

"Pia, tumewapa exposure wachezaji wetu kwa sababu tunatarajia kuiwakilisha nchi kimataifa, haya ni maeneo sahihi ya kuwaleta na kujipima dhidi ya wakubwa wenzetu amabao tutakutana nao kimataifa. Japo ilikuwa ngumu kwa mwalimu kukubali hapo mwanzo, lakini amekuja kukiri mwenyewe kuwa vision ilikuwa maamuzi sahihi kuileta timu hapa Afrika Kusini," amesema Eng. Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live