Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Gamondi akubali kucheza kamari kwa Yao Attohoula

Yao With Gamondi Kocha Gamondi akubali kucheza kamari kwa Yao

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Attohoula Yao namwona akiweza kutumika kama winga wa kulia pale Yanga hata katika michezo mikubwa ama ile ambayo Yanga watahitaji pengine kujilinda zaidi.

Wataweza kuzuia vizuri zaidi huku bado wakiwa na uwezo wa kuwaumiza wapinzani wakati wanashambulia.

Nimesema hivi kwa sababu Yao ana dribbling nzuri ambayo inamfanya aweze kutumika kama namba 7, na tangu hapo anapiga krosi vizuri na ana kasi ya kutosha.

Anaweza kusimama Yao alafu nyuma yake akasimama Kibwana Shomari ama Dickson Job kama kipindi kile pale Manchester United wakati fulani alipokuwa anaweza kusimama Rafael Da Silva kama winga alafu nyuma yake akakaa Wes Brown.

Ama yeye na pacha wake kwa pamoja, Fabio Da Silva aliesimama kama winga wa kushoto alafu Patrice Evra akasimama nyuma yake kwenye mechi ya FA cup dhidi ya Arsenal mwaka 2011.

Au wewe Mwanannchi ungependekeza Yao akacheze eneo gani? Toa maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: