Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Gambia afunguka kupangwa Kundi la Kifo

Tom Saintfiet Kocha wa zamani wa Young Africans ya Tanzania, Tom Saintfiet

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Kocha wa zamani wa Young Africans ya Tanzania, Tom Saintfiet amesema kuwa timu ya taifa ya Gambia imepangwa katika Kundi la Kifo katika Fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023).

Saintfiet ambaye sasa ni Kocha Mkuu wa timu hiyo ya taifa ya Gambia, ameyasema hayo baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutangaza ratiba ya makundi ya AFCON 2023 itakayofanyika Ivory Coast kuanzia Januari hadi Februari mwakani.

Gambia ni nchi ndogo sana na imejikuta ikibananishwa na mabingwa watetezi Senegal katika Droo hiyo iliyofayika Ivory Coast mwishoni mwa juma lililopita. Mabingwa mara tano wa Afrika, Cameroon na Guinea nao pia wamo katika Kundi C.

Timu zote nne zimefuzu kutoka katika hatua ya makundi ya AFCON 2021, ambapo Gambia walicheza Robo Fainali.

“Kweli kabisa sisi ni timu ndogo. Lakini waliona katika fainali zilizopita pamoja na udogo wetu na ukubwa wao, lakini waliona ukali wetu,” amesema Saintfiet.

“Ilitufaa lakini Kundi hili la sasa ni gumu, hakuna shaka tuko katilka Kundi la Kifo, Kundi hili ni gumu zaidi.

“Tunakutana na mabingwa wa sasa wa Afrika, Cameroon ambayo ilicheza Nusu Fainali ya mashindano yaliyopita, na Guinea ambayo ilicheza hatua ya mtoano kipindi kilichopita.”

Gambia ilitolewa na wenyeji Cameroon katika hatua ya robo fainali mwaka 2022.

Ilikuwa ni mechi ya kwanza ya ajabu katika michuano hiyo, ikiwa ni pamoja na ushindi dhidi ya Tunisia na kufuzu kutoka katika kundi hilo. Katika hatua ya kwanza ya raundi ya mtoano waliitoa Guinea, ambayo sasa watakuna nayo tena.

Gamondi akemea ubinafsi Young Africans

“Kwa kweli ni Kundi gumu, lakini ni vizuri tunakwenda kucheza dhidi ya mabingwa wa Afrika na majirani zetu kutoka mkoa wa Sene Gambia,” amesema Saintfiet.

“Katika kipindi cha miaka mitano ya ukocha wangu, na kama kila siku, nimekuwa nikifikiria. Lini tutacheza dhidi ya Senegal?

“Kwa mchezo mkubwa kama huo tunaangalia mbele, na kama ikitokea tumefanikiwa kuifunga Senegal, basi tutaweka historia.”

Saintfiet alianza kuifundisha Young Africans, Julai mwaka 2012 na mwaka huo huo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa CECAFA (Kombe Kagame) na kwa mara ya kwanza klabu hiyo iliweza kutwaa taji mfululizo.

Hata hivyo, Septemba mwaka huo huo baada ya mechi mbili za Ligi Kuu Bara aliondoka Young Africans baada ya kutokea kutoelewana kati yake na uongozi.

Kocha huyo aliiongoza Young Africans kushinda mechi 13 kati ya 16, sare moja na kupoteza mechi mbili.

Fainali hizo zilizosogezwa mbele, baada ya awali kutakiwa kuchezwa katika kipindi cha joto cha mwaka 2023 kutokana na hali ya hewa, zitashirikisha timu 24 na zitaanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024.

Chanzo: Dar24