Michezo ya hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika wikiendi iliopita na kupatikana timu 8 zilizofuzu kwa hatua iliyofuata.
Swali kubwa ni nani atacheza na nani, huku droo ya kupanga michezo ya Robo Fainali inatarajiwa kupangwa Aprili 5.
Kocha mkuu wa timu ya Esperance ya Tunisia, Nabil Maalou amesema yupo tayari kukutana na timu yoyote kati ya National Al Ahly au Js Kabylie,Siyo Simba sports club wekundu wa msimbazi.
Kocha huyo amesema kwa msisitizo kabisa tena kwa utuo kwamba National Al Ahly au Js Kabylie hao waleteni hata Kesho.
Akiongea kiufundi kocha huyo amesema kwamba,ratiba itambeba Simba sports club maana ataanzia nyumbani, kwa hiyo umbali wa kutoka Tanzania hadi Tunisia utamfanya akose muda wa maandaluzi kwa ajili ya mchezo wa marudiano nchini Tunisia.
Simba sports club kama watapata matokeo mazuri katika Mchezo wao katika uwanja wa (nyumbani) machinjioni taifa hawawezi kuhitaji maandalizi makubwa sana, kama timu iliyopoteza mchezo.