Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Esperance ang'atuka kisa boli halitembei

F7dFG UXUAAC 3H.jpeg Kocha Esperance ang'atuka kisa boli halitembei

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Esperance De Tunis, Mouln Chaàbani amejiuzulu baada ya maandamano ya mashabiki wa timu hiyo wakidai kutoridhishwa na kiwango cha timu yao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Chini ya Chaàbani Esperance imecheza michezo miwili ya ligi ya Mabingwa na kufunga bao moja tu, akishinda 1-0 dhidi ya Douanes ya Senegal na mchezo wa pili kutoka suluhu.

Hata hivyo, katika Ligi Kuu ya Tunisia, Esperance wanashika nafasi ya pili katika kundi B wakiwa wamecheza mechi 4, wakishinda 3, sare 1 na kuvuna pointi 10 sawa na Monastir wanaoshika nafasi ya kwanza wakitofautia idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live