Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Eriksson: Nimebakiza mwaka mmoja wa kuishi

Eriksson (15).jpeg Kocha Eriksson: Nimebakiza mwaka mmoja wa kuishi

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson amesema amebakisha mwaka mmoja kuishi baada ya kugundulika kuwa na saratani isiyotibika.

Eriksson, 75, alikuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa England na aliiongoza nchi hiyo kufika robo fainali za Kombe la Dunia 2002 na 2026 na michuano ya Euro 2024.

“Ukipata meseji kama hiyo, unathamini kila siku na unafurahi unapoamka asubuhi na unajihisi sawa, kwa hivyo ndicho ninachofanya,” Eriksson amekiambia kipindi cha BBC World Sporting Witness.

Eriksson, ambaye amefundisha kabumbu kwa miaka 42 aligundlika kuwa na saratani mwaka mmoja uliopita na aliacha majukumu yake ya hivi karibuni ya ukurugenzi wa michezo katika klabu ya Karlstad ya Sweden miezi 11 iliyopita kutokana masuala ya afya.

Klabu alizofundisha ni pamoja na Degerfors na Gothenburg za Sweden, Benfica ya Ureno, Roma, Fiorentina, Sampdoria na Lazio za Italia akitwaa mataji kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live