Kocha wa Klabu ya Dodoma Jiji, Melis Medo ameomba radhi kwa kitendo cha kumpokonya mwamuzi wa kati kadi ya njano kisha kumuonesha kadi hiyo mwamuzi wa akiba.
”Kocha wetu ndugu Melis Medo anaomba radhi kwa waamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu na wadau wote kwa ujumla kutokana na kitendo alichofanya cha kumpokonya kadi ya njano muamuzi wa kati na kumuonesha kadi hiyo muamuzi wa akiba (Fourth Official) katika mchezo namba 185 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Dodoma Jiji.”
”Ukiachilia mbali kuwa kitendo kile ni kinyume na kanuni za Ligi, lakini pia hakikua kitendo cha kiuungwana. Nimekosea, naomba radhi kwa waamuzi wa mchezo ule, Uongozi wa Bodi ya Ligi, Uongozi wa Dodoma Jiji pamoja na wadau wote wa soka,”- Medo
”Aidha Kocha Medo anapenda kuujulisha Umma kuwa amemuandikia barua Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuomba radhi kwa kitendo chake hicho.”