Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Dodoma Jiji akalia kuti kavu, kuwakosa nyota watano

Dodoma Jiji Watano Dodoma Jiji wanakamata nafasi ya 15

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dodoma Jiji inatarajia kuwakosa nyota watano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold mtanange unaotarajiwa kupigwa kesho jioni katika uwanja wa Liti mkoani Singida.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Dodoma Jiji inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi mbili huku Geita ikiwa na pointi tatu ikishika nafasi ya 12 zote zikiwa zimecheza michezo minne.

Mchezo wa mzunguko wa nne Dodoma Jiji walitoka sare ya kutokufungana na Kagera Sugar mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza huku Geita wakitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars kipute kikipigwa katika uwanja huo huo wa CCM Kirumba.

Kocha wa Dodoma Jiji Masoud Djuma aliwataja wachezaji hao kuwa ni Salim Kihimbwa,Augustino Nsata,Joram Mgeveke na Salumu Ngadu ambao ni majeruhi huku Rajabu Mgalula akiukosa kutokana na kufungiwa michezo mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live