Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Coastal arejeshwa Tanga, roho juu juu

Kocha Tanga Kocha Coastal arejeshwa Tanga, roho juu juu

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa Coastal Union, Yusuph Chipo amethibitisha kupokea wito na uongozi wa timu hiyo akieleza kutojua sababu zaidi, huku akieleza kuwa anahisi suala la matokeo kuwa ajenda kubwa.

Taarifa zinadai kuwa huenda kocha huyo aliyetua kwa Wagosi wa Kaya akitokea Pamba FC iliyomtambulisha nchini huenda akapewa mkono wa 'kwaheri' kutokana na uongozi kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo.

Chipo ameiambia Mwanaspoti kuwa amepokea wito wa katibu mkuu wa timu hiyo kurudi Tanga mara moja japokuwa hajajua hitaji lao na kuahidi ataeleza zaidi baada ya kikao na mabosi wake.

"Sijajua kuna tatizo gani labda matokeo, ila ngoja nifike huko nisikie mimi nilikuwa Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi na Yanga," amesema Chipo.

Katibu mkuu wa timu hiyo Omary Ayoub amesema taarifa hizo si za kweli na kwamba hakuna walipotangaza kuachana na kocha wao.

Amesema hata kama ingekuwa tayari asingeweza kuongea na vyombo vya habari isipokuwa taarifa za timu lazima zianzie kwenye akaunti yao.

"Sasa mimi nikupe breaking news wewe kweli au kwanza nitangaze kwenye akaunti yetu? Amehoji na kufafanua "Kocha niko naye hapa Dar es Salaam hizo taarifa mimi sina na siyo sahihi," amesisitiza Ayoub.

Chipo raia ya Kenya alitua kikosini akichukua mikoba ya Melis Medo ameiongoza Coastal katika mechi 14 akivuna pointi 15 akishika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Chanzo: Mwanaspoti