Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Coastal Union mguu nje, mguu ndani

Lazaro.jpeg Kocha Coastal akalia kuti kavu

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Coastal Union kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu, Mkenya Yusuph Chipo na timu kubaki chini ya kocha msaidizi, Joseph Lazaro, huenda naye akaondoshwa kikosini hapo na kuundwa benchi la ufundi jipya.

Mwanaspoti limepenyezewa taarifa hizo siku chache baada ya timu hiyo kupoteza kwa kuchapwa 3-0 na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku ikielezwa sababu zinazomuondoa Lazaro ni maneno aliyoyasema baada ya mchezo huo kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Coastal na Yanga kabla ya kugeukia ukocha, aliwatuhumu viongozi wa timu hiyo kwa kutotenda haki kwa kumuondoa kocha mkuu (Chipo), siku moja kabla ya mechi akidai hiyo imechangia kupoteza dhidi ya Yanga.

“Haiwezekani wewe una matatizo kila siku, kumuondoa mwalimu siku moja kabla ya mechi sio jambo sahihi, wachezaji wamekosa morali na wapo waliokata tamaa kwa kitendo hicho kwani mpira unataka umoja. kwenye uongozi wa mpira kunatakiwa kuwa na watu wa mpira na nasema hivi ili na timu nyingine wapate somo,” alisema Lazaro, kauli inayoonekana kumgharimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live