Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Coastal Union apewa Mtihani mzito

Coastal Union Pic Kikosi cha Wagosi wa Kaya, Coastal Union

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Coastal Union huenda ukampa timu hiyo kocha wake wa sasa, Fikiri Elias endapo tu itabaki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka ndani ya timu hiyo zilieleza kama kikosi hicho kitaendelea kupata matokeo mazuri chini yake basi huenda wakampa kuifundisha kwa msimu mwingine zaidi na wasitafute kocha mpya.

"Hatuko sehemu nzuri sana kwa sababu bado tunapambana na janga la kutoshuka daraja hivyo kama ataibakisha timu kwa michezo iliyobaki basi viongozi huenda wakamuongezea mkataba mwingine tena," kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa Fikiri akizungumzia suala hilo alisema malengo yake kwa sasa ni kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.

"Ni mapema sana kuweka wazi juu ya hilo kwa sababu bado tuna michezo mingi na mikubwa inayotukabili mbele yetu hivyo nadhani baada ya msimu kuisha ndipo tutakuwa na wigo mpana wa kujadili juu ya hilo," alisema.

Kocha huyo tangu alipoongezwa kwenye benchi la ufundi kusaidiana na Joseph Lazaro kikosi hicho kimeshinda michezo yote miwili kikianza dhidi ya Mbeya City Februari 18 na Tanzania Prisons Februari 25 zote bao 1-0.

Fikiri anaiongoza tena timu hiyo leo katika mwchi dhidi ya Singida Big Stars kwenye Uwanja wa Mkwakwani huku ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mabao 2-1, katika mchezo wa kwanza zilipokutana Desemba 7, mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live