Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Chelsea afuta likizo kisa kipigo cha bao 4

Pochettino Chelsea Utoto.png Kocha Chelsea afuta likizo kisa kipigo cha bao 4

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Newcastle United, wikiendi iliyopita kocha wa Chelsea anadaiwa kufuta mapumziko ya siku mbili kwa wachezaji wake ikiwa ni moja ya adhabu kwa kiwango walichokionyesha kwenye mechi hiyo.

Pochettino alikuwa akitazama mechi hii akiwa jukwaani ikiwa anatumikia adhabu yake na akashuhudia mvua hiyo ya mabao huku staa wake Reece James akitolewa nje kwa kadi nyekundu. Baada ya mechi Pochettino alisema ameongea na wachezaji wake na kuwaambia wanatakiwa kwenda hotelini moja kwa moja na kulala na baada ya hapo kesho yake asubuhi (jana), waanze mazoezi ikiwa ni tofauti na utaratibu wa kawaida ambapo baada ya mechi huwa wanapumzika kwa siku moja au mbili kisha ndio huanza mazoezi.

Kocha huyu alisema mechi kama hizi huwa zinampa hasira sana, jinsi wachezaji wake wanavyocheza hawaonyeshi kama wanataka kitu. “Hatuwezi kucheza aina hii ya mpira, Newcastle haikuwa inatisha lakini ilipata ushindi kirahisi sana mbele yetu, tulitakiwa tuwaonyeshe kwamba sio rahisi kutufunga, lakini badala yake ilikuwa rahisi, jinsi ambavyo mabao yalivyokuwa yanaingia na jinsi tulivyokuwa tukikaba, hatukuwa tunaonyesha kwamba tunapambana kwa ajili ya kitu flani muhimu.“

“Inatakiwa wachezaji wakue kiakili, timu kubwa inatakiwa kupambana na kushinda kila wiki. Wachezaji wanatakiwa wacheze kwa nguvu zao zote, ilinikera na ilikuwa ngumu kwangu kutazama mechi, nilikwazika kwa sababu hatukuonyesha kama tupo mchezoni, tulirudisha na kufanya ubao usome 1-1, ulikuwa ni wakati mzuri wa kupata mabao mengine lakini mwisho hatukuonyesha kupambana kwa nguvu, ulikuwa ni mchezo mbovu zaidi kwetu kucheza msimu huu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live