Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Cameroon atupiwa virago mwezi mmoja baada ya kuajiriwa

Marc Brys.jpeg Aliekuwa Kocha wa Cameroon, Marc Brys

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka nchini Cameroon linaloongozwa na Samuel Eto’o limemfuta kazi Kocha Mkuu Marc Brys ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa.

Marc Brys aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu Aprili 9,2024 na Wizara ya Michezo ya Cameroon na kuleta mgongano kati ya Wizara hiyo na Shirikisho la soka la Cameroon.

Kufukuzwa kwa Kocha huyo kumeleta vita kati ya Eto’o na Wizara ya Michezo kila upande ukionyesha kuwa ndio wenye haki katika maamuzi ya kumleta kocha mkuu.

Cameroon inaweza kukumbana na rungu la FIFA baada ya kuipatia siku saba kusuluhisha mgogoro uliopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live