Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha CR Belouizdad aingia darasana kuwasoma Aucho, Bacca na Pacome

Aucho Pacome Bacca Aucho, Bacca na Pacome.

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa aarifa za kiufundi za baadhi ya wachezaji hatari wa klabu wa Yanga SC tayari zimekabidhiwa kwa kocha mkuu wa CR Belouizdad, Marques Paquetta kwaajili ya kutafuta dawa ya kuwazuia wasiigharimu timu yao katika mchezo ujao wa CAF Champions League Jumamosi hii pale Benjamin Mkapa Stadium.

Majina yaliyomfikia kocha Marques Paqueta ni zaidi ya matatu lakini yaliyowekewa msisitizo ni majina ya beki Mtanzania Ibrahim Bacca, kiungo mahiri Mganda, Khalid Aucho, pamoja na Pacome Zouzoua.

Yanga na Belouizdad watakuwa dimbani kesho kukipiga katika mchezo wa raundi ya tano ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Je, unadhani CR Belouizdad wataweza kuwazuia nyota hawa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: