Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha CR Belouizdad: Yanga ni wazuri, wanapenda kucheza soka kama sisi

Marcos Paqueta Cr Marcos Paquetá.

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa CR Belouizdad, Marcos César Dias de Castro maarufu kama Marcos Paquetá (65) amesema kuwa anawaheshimu Yanga SC kwani wanayo timu nzuri na kocha mzuri hivyo mchezo wao wa kesho utakuwa mzuri pia.

Mbrazil huyo amesema hayo wakati wa mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi, Faebruari 24, 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 jioni.

“Nina furaha kwamba hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, ninaamini mchezo utakuwa mzuri na mashabiki watafurahia. Ninajua Tanzania kuna timu nzuri na Yanga wana timu nzuri, wanapenda kucheza soka kama sisi ninaamini kila mmoja atafurahia mchezo huu.

“Tangu mwanzo niliona kundi letu ni gumu, sio kundi ambalo mtu anaweza kusema anashinda kabla mechi hazijamalizika. Tumejaribu mechi baada ya mechi lakini mechi ya kesho ni muhimu kwetu.

“Tulishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga lakini kwa sasa ni hali tofauti na mazingira tofauti. Tuko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, malengo yetu ni kufuzu na si kingine,” amesema amesema Marcos Paquetá.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live