Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha CR Belouizdad: Nimekuja na kikosi imara

Cr BelouizdadcO.jpeg CR Belouizdad.

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa kikosi cha CR Belouizdad cha Algeria Marcos Paqueta amesema hii ni mara yake ya kwanza kuja Tanzania ila hawezi kusema ni mgeni kwa sababu amekuja na kikosi imara anachoamini kitampa matokeo katika mchezo wao dhidi ya Yanga SC, Jumamosi.

“Tutakuwa na takribani siku tatu za maandalizi hapa (Tanzania) kutokana na hali ya hewa inanilazimu kuongeza vitu vingine kwa wachezaji wangu.

“Yanga SC ni timu kubwa ni timu iliyofika fainali la kombe la shirikisho msimu uliopita, hatuwezi kuwachukulia poa na kuna msemo nimeambiwa kuwa hapa kwa Mkapa timu nyingi ni ngumu kupata matokeo ila mimi pamoja na benchi langu tumekuja kulibadilisha hilo,” alisema Paqueta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live