Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Brazil atimuliwa kazi baada ya kumpiga kichwa mwamuzi wa kike

Kocha Yamemkutaaa Kocha Brazil atimuliwa kazi baada ya kumpiga kichwa mwamuzi wa kike

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA wa Klabu ya Desportivo Ferroviaria inayoshiriki daraja la tano nchini Brazil Rafael Soriano ametimuliwa kazi baada ya kumpiga kicwa mwamuzi wa pembeni na kusababisha kumpasua pua.

Tukio hilo limetokea katika pambano la robo fainali kati ya Desportivo Ferroviaria dhidi ya Nove Venecia ambapo Nova walishinda kwa jumla ya mabao 3-1.

Kocha wa Desportivo Rafael Soriano aliingia uwanjani baada ya kipindi cha kwanza kumalizika akienda kupinga maamuzi ya mwamuzi wa kati wa mchezo lakini mwamuzi msaidizi mwanadada Marcielly Netto akaingilia kati ili kumzuia ndipo hapo alipoambulia ndoo ya maana na kupasuka pua.

Mara baada ya tukio hilo Klabu ya Desportivo Ferroviaria ilitoa taarifa ya kumtimua kazi kutokana na kitendo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live