Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Biashara ataka wachezaji wake waheshimiwe

57f98c9399b37c85676a84476437fd6d.jpeg Kocha Biashara ataka wachezaji wake waheshimiwe

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa timu ya Biashara United, Patrick Odhiambo amesema kuwa wachezaji wake wanastahili heshima kwa jinsi walivyopambana na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo na kuivusha timu hiyo hadi hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Biashara United walitoka kupoteza 2-0 ugenini dhidi ya Azam FC, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, walikuwa na siku moja ya kujiandaa baada ya kuwasili Musoma Mei 22, ambapo walifanya mazoezi kwa dakika 20 pekee kabla ya kesho yake kuwavaa Namungo FC.

Akizungumza na gazeti hili, Odhiambo alisema kuwa amefurahia kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake na kupata matokeo mazuri, ingawa haikuwa rahisi kutokana na kupitia wakati mgumu kwa kutopata muda wa kutosha wa kufanya maandalizi kutokana na kutumia muda mrefu njiani kutokana na kutumia usafiri wa basi.

“Tulikuwa na wakati mgumu kujiandaa na mchezo huu, hakika ni jambo la kufurahia vijana wangu wamefanya kazi kubwa hatukuwa na muda wa kupumzika tumetembea umbali mrefu bila kupumzika.

“Malengo yetu ni michuano ya kimataifa ili tupate uhakika tunapaswa kushinda taji hili, huku tukiendelea kupambana katika Ligi Kuu pia ili kuhakikisha tunamaliza ndani ya nafasi ya nne,” alisema Odhiambo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz