Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Belouizdad achanganyikiwa na Pacome

Aziz KI X Pacome Kocha Belouizdad achanganyikiwa na Pacome

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Kocha wa CR Belouizdad, Marcos Paqueta akianza kukumbana na presha ya kupoteza kazi ameondoka, huku akimlalamikia kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua na Stephanie Aziz KI ndio waliowaharibia timu yao na kupata kipigo kikubwa.

Akizingumza na Mwanaspoti Paqueta alisema hatua ya viungo wake na mabeki kushindwa kumdhibiti Zouzoua lilikuwa kosa kubwa lililowapa wakati mgumu kwenye mchezo huo wa juzi ambao Yanga ilishinda mabao 4-0.

Paqueta alisema Pacome alikuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo na mapema walishajipanga kumdhibiti lakini hesabu zao hazikufanikiwa kutimia baada ya awali kushtukia makali yake.

“Yule mwenye jezi namba 26 (Pacome) ndiye aliyefanya kazi kubwa kwenye mchezo huu, alituweka kwenye wakati mgumu sana licha ya kwamba tulishajipanga kuhakikisha hafanyi kazi kwa utulivu,” alisema Paqueta raia wa Brazil.

“Alikuwa na makali kila alipogusa mpira kuelekea lango letu, ana akili na kasi, kwangu Mimi tulifanya makosa kutomdhibiti leo (juzi). Mbali na Zouzoua pia Paqueta amemtaja kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephanie Aziz KI alikuwa hatari na mipira yake ya kupenyeza.

“Yule mwenye jezi namba 10 pia (Azizi Ki) alikuwa na mchezo mzuri, alikuwa na pasi za hatari kwenda kwenye eneo letu la ulinzi, tulifanya makosa mengi yaliyotugharimu.”

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: