Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Belouizdad: Yanga watumie mtaji wa mashabiki wao kesho

YANGA MASHABIKI ER.jpeg Kocha Belouizdad awataka Yanga watumie mtaji wa mashabiki wao kesho

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa CR Belouizdad, Marcos César Dias de Castro maarufu kama Marcos Paquetá (65) amesema wapinzani wao Yanga SC, wanao mtaji mkubwa wa mashabiki hivyo wanapaswa wawatumie vizuri kwenye mchezo wao wa kesho.

Mbrazil huyo amesema hayo wakati wa mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi, Faebruari 24, 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 jioni.

“Yanga watakuwa nyumbani na wana mtaji wa mashabiki, wanatakiwa wautumie vizuri mtaji huo kwa ajili ya mchezo huo. Sisi tumejiandaa na hilo, tunacheza na moja ya timu imara, wachezaji wao wanacheza vizuri sana kama ambavyo walifanya kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi yao,” amesema Paquetá.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: