Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Bafana aichana ligi Sauzi

Hugo Broos LL Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos ameliweka soka la Afrika Kusini katika ramani ya dunia, lakini ameonya kwamba Ligi Kuu ya nchi hiyo inapaswa kuboreshwa ili kuinua vipaji vya nyumbani.

Broos amejibu waliokuwa wakimponda kwa kuipeleka Bafana katika nusu fainali yao ya kwanza katika miaka 24.

“Kwa hiki kilichotokea soka la Afrika litaanza kuchukuliwa siriaz, lakini Ligi Kuu ya PSL bado inatakiwa kuboreshwa,” alisema.

Kocha huyo mzaliwa wa Ubelgiji alisema kiwango kilichoonyeshwa na Bafana hadi kufika nusu fainali yao ya kwanza tangu 2000, ni picha halisi ya Ligi Kuu ya PSL kwa sababu wachezaji 20 kati ya 23 alioenda nao kwenye Afcon wanacheza soka la ndani nchini Afrika Kusini. Hata hivyo, Broos alisema PSL bado inapaswa kuwa bora zaidi.

Broos amekuwa akiwaanzisha hadi wachezaji wanane wa klabu ya Mamelodi Sundowns katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Afrika Kusini huku pia akimjumuisha mchezaji wa tisa, Percy Tau, ambaye pia ameitumikia Mamelodi kabla ya kutua kwa mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri.

“Tumekuja hapa na nadhani kulikuwa na watu wengi sana kule Afrika Kusini ambao hawakuwa na imani na timu hii, lakini sisi tuliiamini. Wachezaji waliamini kwamba inaweza kuwa na imekuwa,” Broos alikaririwa na televisheni ya SABC Sport.

“Nadhani hili ni jambo zuri sana kwa soka la Afrika Kusini. Wachezaji wa Afrika Kusini wako sokoni sasa, hivyo inamaanisha kwamba soka la Afrika Kusini litaangaliwa zaidi,” aliongeza.

Bafana sasa itaivaa Nigeria katika nusu fainali kesho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live