Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam kafumbia jicho eneo hili, litamuumbua

Dabo Kocha Azam kafumbia jicho eneo hili, litamuumbua

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Najua Azam wamefunga usajili wao lakini kwa mtazamo wangu Azam walihitaji Center Back mwingine ikiwezekana hata wawili.

Wapo watatu wa kati, Daniel Amoah, Abdallah Kheri 'Ssebo' na Malickou Ndoye na makeshift ya Edward Manyama ambao waliruhusu mabao 29 ya ligi msimu uliopita, 12 zaidi ya alieruhusu mabao machache zaidi.

Hili daraja unaliunga kwa kuongeza quality. Singida Fountain Gate wana mabeki wanne wa kati lakini wamemwongeza na Joash Onyango kwa ajili ya michuano ya kimataifa. Yanga walikuwa wanne lakini kaongezwa Gift Fred kutokana na potential yake.

Mwaka 2018, Liverpool walikuwa na mabeki wa kati wanne, Joe Gomez, Joel Matip, Dejan Lovren na Ragnar Klavan lakini kwa sababu ya uhitaji bado, wakamwongeza beki wa kati watano, Virgil Van Dijk na ndio akaja akawa karata dume ya Liverpool pale nyuma.

Hakuna kinachotosha hasa kwenye soka na si vizuri kujifunga kwenye kuyatafuta mafanikio ndio maana Pep Guardiola analeta watu kila siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live