Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam bado ana matumaini Chamazi Complex

Lavigne Kocha Azam Kocha Azam bado ana matumaini Chamazi Complex

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wadau wa soka wanaiona kama Azam FC imeshang’olewa kutokana na kipigo cha mabao 3-0 ilichopewa ugenini na Al Akhdar ya Libya, lakini kwa kocha wa timu hiyo, Denis Lavagne, hali ni tofauti kwani bado anaamini atapindua meza wikiendi hii.

Azam inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Azam Complex ikijiandaa na mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku Kocha Lavagne akitamba anaamini vijana wake watapindua meza licha ya aibu waliyiopata ugenini.

Ushindi wa mabao 4-0 ndio utaifanya Azam iiondoshe Akhdar na kusonga mbele na kikosi kizima chini ya Kocha Lavagne wanaamini inawezekana na wameweka mipango mikakati ya kupindua meza hiyo kibabe.

Pamoja na kuweka mikakati hiyo, Lavagne ameeleza katika mechi ya marudiano kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye timu yake kuanzia kwa kikosi, aina ya uchezaji na morali.

“Hadi sasa bado tunajitafuta, hatujawa na kikosi cha kwanza cha kudumu lakini tuna aina ya kila mchezaji. Kila mchezo unakuwa na mbinu zake, mchezo wa nyumbani tunahitaji kushambulia na kutafuta mabao zaidi kwahiyo tutabadilika karibu kila eneo tofauti na tulivyoicheza ugenini,” alisema Lavagne aliyewahi kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008 akiinoa Cotton Sports ya Cameroon na 2021 alipoifikisha JS Kabaiyle ya Algeria fainali ya Kombe la Shirisho Afrika.

Kwa upande wa wachezaji, beki wa kikosi hicho, Nathanael Chilambo ameeleza wanaendelea kujifua ili kuhakikisha wanakuwa bora na kufanya vizuri mechi ijayo.

“Matokeo ya kwanza yalituumiza lakini imetupa funzo na tunajiandaa ili kuwa bora katika mechi ya marudiano,” alisema. Chilambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live