Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam ashtukia jambo

69544 Azam+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam wapo kwenye maandalizi ya msimu mpya, lakini benchi la ufundi la timu hiyo ni kama wameshtukia jambo na kuapa kujipanga ili kila kitu kwao kiende sawa.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Idd Nassor 'Cheche' amesema anatarajia kuona ushindani mkubwa msimu wa 2019/20 kutokana na sajili kubwa zilizofanywa na klabu.

Cheche ameyasema hayo baada ya timu yake kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Cheche alisema haikuwa kazi rahisi wao kufanikiwa kupata ushindi huo na kubainisha kuwa bila mbinu binafsi za wachezaji basi ingekuwa ngumu kwao kupata matokeo.

"Ulikuwa ni mchezo mzuri kwetu kujipima kuelekea mashindano ya kimataifa na Ligi Polisi Tanzania inakikosi imara na cha nyota waliojaa uchu wa mafanikio naamini ligi itakuwa na ubora kulingana na usajili uliofanywa," alisema.

"Tunaendelea kujifua ili kujiweka fiti zaidi ufinyu wa mabao huku tukiwa na safu bora ya ushambuliaji unatokana na uimara wa walinzi wa timu pinzani haina maana kwamba safu yetu ni butu," alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz