Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam anaamini ushindi Libya

Azam FC KIKOSI MBEYA 1140x640 Kikosi cha Azam FC

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Azam FC kimetua salama nchini Libya tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Al Khadar, huku kocha wa washambuliaji wa timu hiyo, Kally Ongala amesema kwa ubora wa kikosi hicho wanaamini wataibuka na ushindi licha ya kucheza ugenini.

Azam itaumana na Al Khadar kwenye mechi ya mkondo wa kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kurudiana wiki ijayo jijini Dar es Salaam na Ongala alisema licha ya mazingira ya ugenini, lakini bado anaamini wana nafasi ya kupata matokeo mazuri kwa jinsi walivyojiandaa tangu wakiwa nyumbani.

“Hesabu zetu ni kufanya vizuri pamoja na kuwa ugenini ili kurahisisha kazi kwenye mchezo wa marudiano, timu ipo katika hali nzuri kimwili na kiakili kwa ajili ya mchezo,” alisema Ongalla.

Azam imetua Libya bila wachezaji saba walioachwa nyumbani kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuwa majeruhi Wilbol Maseke na Kenneth Muguna, huku Twalib Mohamed, Ibrahim Ajib, Aziz Ismail, Shaaban Chilunda na Rodgers Kola ikitokana na ishu za kiufundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live